kalimah.top
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

roma mkatoliki – nipeni maua yangu كلمات اغاني

Loading...

tumek_misi roma
rudi nyumbani
uwatetee wanyonge ndugu zako
uwak_mbushe

verse 1
sasa sijui nianzie wapi kifuani nimebeba mengi
na sitotenda haki nisiposema hiki sipendi
hiki napenda kile sitaki mambo ya kishenzi
tanzania haijaezekwa bati na wamekula pesa ya ujenzi
yaani nchi wanaifanya mti mjenzi anauona mbao
ndege ataona makazi mkulima ataona mazao
mganga atauona dawa na mpishi atauona kuni
ataemiliki mwenye power sisi atatusagia kunguni
na ukisema hawatufai wanakuumiza uwe mpole
yaani wanaangua papai kwa kutumia gobole
mnatumia nguvu kubwa kwenye mambo madogo
jeshi gani mpaka leo mmeshindwa k_mjua kigogo
tukiongelea kutekwa eti tunarudia ajenda
hamjibu mnakwеpa mbona mama anarudia kilemba
nchi gani raia akihoji mnasema anakosoa
na akikosoa anatukana serikali hii sio poa
haya basi tusеme mko sawa na mna nia nzuri na sisi
mbona vyuma vimekaza halafu mama anaificha grease
mara mkapandisha tozo kampeni mkono hatuwaungi
si tulihoji mkajibu kwa dharau tuhamie burundi
tatizo mkishaapishwa tu mnawaza uchaguzi ujao
hamuwazi njia mbadala ya k_mlinda mkulima na mazao
sasa iringa si tuna maitu halafu tuspick twaagiza china
manaake hapo kwanza ncheke yaani bongo kikubwa uzima
sa mnatuambia tujiajiri mbona nyinyi hamkujiajiri
okay nikupe boda yangu kisha we unipe uwaziri
nikukabidhi vyeti vyangu hangaika navyo mwezi mmoja
niko pale nakujgoja uje tuongee lugha moja
mi sio ccm sio chadema hili niliweke wazi
ila ukiweka ccm na andazi ntachagua andazi
simuamini mtawala na mpinzani simsadiki
maana wanaendelea kukatika huku deejay kauzima mziki
na inaniuma kuona msomi wa degree tatu
nashindwa k_mpa ajira sasa anauza nyanya karatu
sasa sijui mtaniua nikimshikia mama shilingi
maana hata inyeshe mvua mnasema anaupiga mwingi
na ninamkubali na nitamng’ata sikio kama hujui
wanaomkosoa ndo wanampenda wanaomsifia ndo maadui
ili wapate teuzi ndo wanamlamba miguu
wakimpamba hawamsaidii amiri jeshi mkuu
chorus
tunakupenda roma tunak_miss roma
rudi nyumbani roma utusemee
tunakupenda baba tunak_miss mwana
tunakuk_mbuka sana

verse 2
hivi hamjasikia tetesi kuwa remote iko msoga
si huku mageng imedoda magogoni imenona
watu tatu ndani ya track moja wamekalia kigoda
ngolo kante anampa mbape cross anafunga pogba
hii nchi ina wenye nchi walanchi na wananchi
na kuendelea kuwachagua ni kwenda na mchanga mbichi
tuwajaribu wapinzani watawala si wameshapata
ugoro umewaingia puani sasa ona wanapiga chafya
wanatumia dollar kubaki kuongoza dola
watawafunga watapora wataua watahonga vijora
karatasi tunaibiwa za kura kwenye sanduku
kwa hiyo mnatuonyesha ziwa huku mmeziziba chuchu
okay kura ziko 300 na kuna watu mia kwa jimbo
na kituoni hakukua na watu halafu wameshinda kwa kishindo
sa kama askofu mfufua watu ameiba kura za wapinzani
je atashindwa kuiba sadaka za kura kanisani
hii ni gani mchungaji akitaka gari twamchangia
muumini akitaka gari anaombewa tunamsalia
sa mchungaji tusimpe pesa tumuombeevna yeye pia
tukae pale tusubiri miujiza ya wagalatia
wabunge wengi mlishinda kwa hisani ya mwendazake
mkipatacho muende chato mk_mbuke hata ndugu zake
jimbo hili haliendelei cause mmemchagua mpinzani
haya sasa mmeshinda kote fauluni huo mtihani
turuhusu siasa za amani turudi zile enzi zetu
uchaguzi sio siku moja ni mchakato wa muda mrefu
mikutano ya nje na ndani ndo tunaimarisha chama
daily mtulishe majani halafu sikukuu mtupe shawarma
keki ya taifa ni kubwa tuache siasa za risasi
mnawaonea wakishika dola watalipa kisasi
tulipotoka ni mbali siasa za mwendazake
msirudi msilale chali huku mnatutemea mate
na basata msikie hili msije fungia huu wimbo
kichwa kisicho na akili ni mzigo kwa shingo
sawa tulinde maaduli ila tusiue wabunifu
mtupende tunaokosoa kama mpendavyo wanaosifu
wengine wamekuwa viongozi na mliwaona tu marapper
hiphop ni mkombozi na sauti isiyo na mipaka
ushauliza kwanini bega lipo karibu na kwapa
usiondoke baki hapa usikie verse inayofuata
chorus
tunakupenda roma tunak_miss roma
rudi nyumbani roma utusemee
tunakupenda baba tunak_miss mwana
tunakuk_mbuka sana

verse 3
nawashangaa vijana warembo na watanashati na nusu
wanaosema bila mlengo eti siasa haiwahusu
mwanasiasa anaweza amua tu na ukalala mahabusu
mnakosea wadogo zangu na kamwe sitoruhusu
siasa ndo inaamua sukari iuzwe shingapi
na inapanga kaliua ni wapi wajenge zahanati
na ijue tofauti ya mwanasiasa na mwanaharakati
mmoja ndo mzalendo mwingine maslahi binafsi
ntawafundisha kitu kabla hajawika jogoo alfajiri
pesa unayonunua maduta mkate unaolipa bili
hoja yake inamlipa raisi polisi mbunge waziri
so una haki ya kuwakosoa maana we ndo umewaaajiri
tatizo hatuna ujasiri na akili tumekaza fuvu
vipi nitafuzu kichwa suzuki engine ya isuzu
anayechelewesha msafara siku zote ni ng’ombe wa mbele
ila anachapwa wa nyuma na ndo anayepiga kelele
na mjenga katiba mpya sio bawacha wala bavicha
eti wabonngo maji sio katiba mnawaficha
haya sasa hayo maji yako wapi mbona hamuongei
uko wapi umeme mmebugia kiazi cha mtoto
mdomo unacheza sebene
katiba iliyopo ni bora ipa ni bora kwa watawala
ukipinga wanakupa keai na hauna hela kibatala
kwa mwamvulu wa maendeleo wanahairisha mchakato
mbona mkoloni alijenga miundombinu yote hapo
na ili nchi iendelee inahitaji vitu vinne tu
uongozi bora, siasa sadi, ardhi na watu
yanga na simba ni wapinzani ila sio kwamba hawapatani
maji yanayotoka mto msimbazi ndo yanayojaza jangwani
na hiyo ndo amani tuitakayo sisi sio vurugu
tunataka kuona januari anamgongea fegi sugu
hakika naacha glasi ya bapa mezani anaenda msalani
anamuachia mwigulu anarudi na anakunywa kwa amani
na sio utani msipojifunza hapa ndo basi tena
aliyesema aomgezewe muda bungeni ndo ameaga mapema
wakamlisha asali kwa kisu akalamba akamwaga wino
tangulia na dereva barua utaikuta chamwino
mi nitakufa mimi ila ngoma zangu zitaishi
na mtakuja na mashada siku yangu ya mazishi
nipeni maua yangu niy_n_se angali nipo hai
nikiondoka mnik_mbuke msilie bali mfurahi
chorus
tunakupenda roma tunak_miss roma
rudi nyumbani roma utusemee
tunakupenda baba tunak_miss mwana
tunakuk_mbuka sana

كلمات أغنية عشوائية

اهم الاغاني لهذا الاسبوع

Loading...