kalimah.top
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

fid q – 11. kiberiti كلمات اغاني

Loading...

(lu, lu, luffa!)

[verse 01] fid q
haueleweki hata uki_shine kwa punchlines on facebook
haiwi_fine ka′ rayvan, we’ fake tu
sikuoni b.e.t au mtv wak_play tunes
miaka nenda we′ msanii, mc una play tu
makida, we’ sio king kama kiba
sio yao ming kwenye ring
mistari mingi zaidi ya zebra? (zaidi ya zebra!)
un_z_ngua n_gga, haujajijua n_gga
umeangukia pua, bishoo hauwezi kuwa jigga
rent mwezi ujao na haujalipa school fees
ya mwanao, unaumiza kichwa ewe q_fid
’til now hauioni future, we′ stupid
hauj_piga bao na kutwa unawaza groupies?
pengine ni nuksi umejiletea au chuki umejijengea
hauk_mbuki ulipotokea bro (bro)
wabaya mauzushi, wanayachochea
haushtuki ushapotea
wakushi wanakutetea bro
unakosea bro, ni kweli hauna spea bro
ku_play fair, ikuwachеzea ikatokea droo
sikutegеmea bro, hatuwezi hataku′onea bro
tushajionea ulivyo mlevi, ukaikosea show
[chorus] saida karoli
kiberiti, ninakuona unavyoniwashia moto mie (aye)
kiberiti, ninakuona unavyoniwashia moto mie (aye)
ayi, ma_mama, kiberiti ayi, ma_mama

[hook] fid q
nikiwa alone in my room, sometimes i stare at the door
and in the back of my mind, n_z_ita hisia hebu njoo zinaingia zinaniambia hii dunia ni soo
haiko sweet kama dove, i see, i need love

[verse 02]
tazizo lako hautaki kuuza maneno
legeza ka’ wenzako acha kutukuza misemo (kutukuza misemo)
sheria ni yako ila isiuache msumeno
ukijikuna tako, usikate kucha kwa meno
ongea usikike au kaa kimya usidharaulike
au utupishe na jina lisahaulike
tulazimike kuzima ili itulipe gwajima tumuite
aje kukupima heshima ya bash_te
nje ya town, show huwa zina cloud ya kiwaki
kaza crown ibaki, ukikaza sana hawataki
tunajua una uwezo wa juu na kismati
na haujawahi kupigwa bu! basi unajiona tupac
kabla ya rotten brothers ulikua na chepe
two nature boys ndiko ulikoanza makeke
mwaka huu, mwaka we mwaka
ikakuweka juu ikawa q hakuna asiyemtaka
well, lini uta_retire urudi kuuza mtumba lango?
una roho mbaya, hadi leo haujamk_mbuka rado
we′ sio kichwa, we’ unaweza fichwa
ikichorwa hip hop, siioni sura yako picha
[chorus] saida karoli
kiberiti, ninakuona unavyoniwashia moto mie (aye)
kiberiti, ninakuona unavyoniwashia moto mie (aye)
ayi, ma_mama, kiberiti ayi, ma_mama

[interlude] saida karoli & fid q
fid q nikuulize, hivi?
siri yako nini kuishi kwenye game muda mrefu, eh?

kwanza unajua, mi′ huwa sichukulii vitu personal ukiniponda sichukulii personal
ukinisifia sichukulii personal
ni’chojifunza ni kwamba usichukulie kila kitu personal
na zaidi, ufunze ubongo wako kung′amua jema kwenye situation yoyote ile
na hivi ndio vitu ambavyo don miguel kwenye kitabu chake cha the four agreements ameviongelea
kwa mfano, nikikutana na wewe sokoni au kokote na nikakuambia, “wewe ni mjinga” wakati hata sikujui, na siku hiyo hiyo ndio mara ya kwanza tumeonana anaekua amevurunda hapo sio wewe ni mimi
so kwa wewe kuchukulia personal na ku_react
ni sawa kuwa umekubaliana kihisia na jina hilo la mjinga
na huenda ukanifanya nijione mimi ni muoteaji mzuri
kuchukuria kitu personal ni kukubaliana moja kwa moja na kilichosemwa
na kama kweli umekubaliana inamaana kimekuingia na kinapokuingia husambaza sumu ambayo huziua zile fikra chanya ulizokuwa nazo na kufanya usichukue maamuzi sahihi
kila mtu anafanyanya vitu kwa ajili yake na kwa faida anazozijua yeye mwenyewe
ni mara chache sana wewe kuzing’amua hizo faida binafsi za watu
wengine utaona ni kwa ajili ya attention wengine ni kwa sababu inawaingizia kipato
wengine iyo kitu huwaacha tu na furaha ya moyo na vitu kadhaa wa kadha
kila mtu ana ndoto zake na pia hupendelea kufanya vile akili yake inamtuma
na pengine dunia tunayoishi sisi sio dunia wanayoishi wao
hivyo tunavyochukulia vitu personal ni sawa na kuwa_ kuwaaminisha ya kwamba tupo kama wanavyotufikikiria
na tunaota kuwa na utulivu kama walionao wakati sio kweli
na hata tusi liwe la nguoni kiasi gani
ni vyema ukajua na kuamini ya kwamba halikuhusu
k_mbuka limjaalo mtu ndilo limtokalo
wengine wameathiliwa na malezi waliopitia pamoja na makuzi kwa ujumla
so, hata mtu akiniambia we, yani
kwa mfano mtu akikwambia, “we saida ni mshamba kuliko wasanii wote tz”
ni vyema ukamsamehe tu!
he! lakini k_mbuka k_msamehe mtu inamaana alikukwaza uka_mind ndio maana ili usimfugie chuki na hasira
ndio maana inabidi umsamehe
na k_mkasirikia inamaana uliruhusu ile sumu ikuingie kwa hiyo kwenye hili mtu akikwambia, “wewe ni mshamba kuliko wasanii wote”
tunashauriwa k_muacha kama alivyo tu kwa sababu hizo ni hisia, imani na maoni yake yeye binafsi
na dawa pekee ya kuituliza iyo sumu
ni kuwapotezea tu ili waendelee kupambana na hali zao
watu wengi huwa wanashindwa k_mjaji mtu kama alivyo kutokana na vitu alivyonavyo
cha ajabu mentality hii imetupelekea sisi kuacha au kusahau kabisa kuchukulia vitu kama vilivyo na kuanza kuvichukulia kama tulivyo
[chorus] saida karoli
kiberiti, ninakuona unavyoniwashia moto mie (aye)
kiberiti, ninakuona unavyoniwashia moto mie (aye)
ayi, ma_mama, kiberiti ayi_yi, ma_mama

[outro] saida karoli
ninashangaa k_mbe wanadamu ndivyo walivyo
k_mbe wanadamu ndivyo walivyo
ayi, ma_mama ayi_yi, ma_mama
ninashangaa k_mbe wanadamu ndivyo walivyo
k_mbe wanadamu ndivyo walivyo

كلمات أغنية عشوائية

اهم الاغاني لهذا الاسبوع

Loading...