kalimah.top
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

alex mwakideu – mahaba haba (shairi) كلمات اغاني

Loading...

ni juzi tu tulipokutana
mimi na yule msichana
mkahawani tukapelekana
chai maandazi na mbaazi tukalishana
mapenzi yetu mbuga yakachana
na kwa mambo yote tukaelewana
ona sasa wataka kuwachana
na hata wazazi wetu hawajakutana

usinipeleke raba na mahaba yako haba

wak-mbuka jumamosi ya tarehe saba
ile siku tulikutana saba saba
tukajivinjari kwa siku saba
wiki nzima hotelini katika kila chumba cha saba
malavidavi yakawa ni kwako tu habuba
zawadi nazo nikanunua tena zile babu kubwa
sasa nasema twende kwa baba kule malaba
kisha wasahau yangu yote mahaba

usinipeleke raba na mahaba yako haba

mwenzio nataka mapenzi ya kuaminiana
mimi na wewe kushikana
bega kwa bega tukiandamana
mungu akitujalia tupate na wana
moja kichuna aiitwe jina la mamako ana
na mwingine kijana tumwite baba mzee chuna
sio tu kila siku starehe za gharama
na hali wewe mwenyewe hata peni huna

usinipeleke raba na mahaba yako haba

namalizia nikikusihi uwache pupa
usije ukayatupa mapenzi kwa pipa
utamu wa mapenzi ni kulipa
nikikupa na wewe wanipa
angani mwenzangu tutapaa
na chochote utakacho nitakupa

kwa hio tulia upate utamu hapa
hamna haja tena ya kutapa tapa

usinipeleke raba na mahaba yako haba

skiza albamu ya mahaba
na ujifunze mwenzangu habuba

كلمات أغنية عشوائية

اهم الاغاني لهذا الاسبوع

Loading...