kalimah.top
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

zuhura shaban - kama ni rahisi lyrics

Loading...

kama ni rahisi

kama ni rahisi ungelianza ili kuyatenda
sina wasiwasi wakuyapoteza niliyoyaunda
natoa nafasi kwa anayeweza aje kunishinda
ameshanihisi kwake napendeza ndiyo kanipenda

aliponitaka ili niwe wake sik_mhofia
sikuwa na shaka hilo ombi lake nimelipokea
sikubabaika tangu anitake nimeshatulia
sitobadilika naipata kwake raha ya dunia

kama ni rahisi ungelianza ili kuyatenda
sina wasiwasi wakuyapoteza niliyoyaunda
natoa nafasi kwa anayeweza aje kunishinda
ameshanihisi kwake napendeza ndiyo kanipenda

mapenzi adhimu yasiyo mithali yameniingia
tena ni matamu kuliko asali nayafurahia
walonilaumu potelea mbali leo nawaambia
sitojidhulumu kwa w_ngu mpenzi nikaangaamia

kama ni rahisi ungelianza ili kuyatenda
sina wasiwasi wakuyapoteza niliyoyaunda
natoa nafasi kwa anayeweza ajе kunishinda
ameshanihisi kwake napendеza ndiyo kanipenda
nimemuamini ni w_ngu mlezi anayenileya
w_ngu wa moyoni tena namuenzi namnyenyekea
nakula yamini pendo sigeuzi nimeswafi nia
uovu asilini kwa w_ngu mpenzi sitomtendea

kama ni rahisi ungelianza ili kuyatenda
sina wasiwasi wakuyapoteza niliyoyaunda
natoa nafasi kwa anayeweza aje kunishinda
ameshanihisi kwake napendeza ndiyo kanipenda

toka awe w_ngu nami niwe wake kigiuu na njia
mara mje kw_ngu mara mwende kwake fitina kutia
hili pendo langu kwake liondoke mmedhamiria
yabaki machungu kisha mtucheke na kuhadithia

kama ni rahisi ungelianza ili kuyatenda
sina wasiwasi wakuyapoteza niliyoyaunda
natoa nafasi kwa anayeweza aje kunishinda
ameshanihisi kwake napendeza ndiyo kanipenda

mtafanya nini, mtafanya nini?
pendo letu la wawili nyie lawaudhi nini nyie?

mtafanya nini, mtafanya nini?
penzi letu la wawili linawaudhi nini nyie?
umbea unakazi eleweni mafitina
kazi yenu uchochezi
lengo lenu tuachane

si mikiki si biriti lilomlewesha bwana nyie

mtafanya nini, mtafanya nini?
penzi letu la wawili nyie lawaudhi nini nyie?

kama munadhani ni rahisi mungeanza kuyaunnda
mimi sina wasiwasi najiamini napendwa
naye kw_ngu kajihisi ndomana ameniganda mimi

mtafanya nini, mtafanya nini?
huba zetu za halali zinawakata maini
mumeona twapendana roho zinakuumeni
wapenzi tumeshibana hatujali mafitini
pendo letu limefaana linawakata maini nyie

mtafanya nini, mtafanya nini?
hamuezi kutuzidi tushakolea pendoni sie
mtafanya nini, mtafanya nini?
pendo letu la wawili nyie lawaudhi nini nyie?
©shariff kombo _254 743 144 211

كلمات أغنية عشوائية

اهم الاغاني لهذا الاسبوع

Loading...