kalimah.top
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

wakazi - amka mtanzania كلمات الأغنية

Loading...

songa
yeah! innocent aah
songa yeah aah
habari mpendwa,mlengwa wa hii habari/
kabla hujatendwa jaribu kwenda na tahadhari/
jali kalenda,kuna chenga za hatari/
usipojijenga basi utatengwa na safari/
usione noma wauza sura hawana ishu,kila siku soma pia chana kama chiku/
uza mahindi maji baridi misosi mingi/
jua la utosi usihofu wee force king/
ukungu unajaa kitaa utundu balaa/
utashangaa sister duu kadata na mzungu kichaa/
punguza makuu muda ndio huu fanya balaa/
acha tamaa hizi zama za njaa/
mabucha yamechacha nyama za mwili haziridhishi/
ishi ki culture na usafiri wa marafiki,akili ni ngao/
chart ni usafiri ambao/
unawashusha kikatili wasafiri kibao/
acha tamaa hizi njama za njaa,punguza makuu muda ndio huu fanya balaa/

zaiid
ki to the ja to the na
fahamu mi ndio salama kupita cheichei/
haya maisha dojo huwa sensei kisha jifunze zaidi fikra hazij_panda bei/
mi somo darasa wee ni pono nakuhasa kikomo mashaka stuka hata babu alikuwa kaka/
maisha sio kamali ila mali maarifa kwenye hali bila zari kutafuta yataka sifa/
mama alichofanya kukuzaa pata butwaa moyo haukutupi unasinyaa/
usiwe kkb kula kulala bure uwe jkt elimu kupita shule/
ishi kwa malengo usiishi kwa mapengo,ubishi ukija ubichi ni bichi isiyo na upendo wee jibu ni kuishi ishi inavyoishi dunia/
zunguka kama sayari,ukisimama utaumia/
p the mc
wow aah
bongo mashaka hali sasa ni hatari/
tufanye fasta ili muafaka tuuweke shwari/
acha utata kisa una madaraka kiserikali ufanye unachotaka weka mipaka usifike mbali/
mvi kichwani utadhani mwenye busara k_mbe kutwa na vitoto gizani kwenye misala/
kutwa uchumi fyongo bongo haiwezi kupumua/
k_mbe nyie ndio makamongo michongo mnaitibua/
pesa za bajeti zinaishia kwa vibinti/
vuta hisia watanzania watatoka vipi kwenye hili janga la uf_kara uliokithiri/
giza limetanda haki imelala kwa matajiri aah/
usifanye pesa fimbo kwa wasiojoweza ndio maana wengi wanasepa marekani uingereza/
maana hali ikinesa si ndo wanaotupoteza hapa hakuna cha kuteta huu ndio ukweli nakueleza/
usiwe kkb kula kulala bure uwe jkt elimu kupita shule/

wakazi
aaah
picha inaanza mjuba unakwea pipa kisha ukiliwaza kialinacha kabla ya kufika/
uhondo wa ndoto ndio uongo wa ndoto ingawa kiukweli nyuzi joto kiwanja si kama bongo/
mbeba box yeah nia yangu ki make yeah/
msosi utapata haimaanishi kula feki jisahau uko kwa watu usiishie kogonga fegi na kisha kurudi home bila hata begi/
dunia ya sasa ujasiriamali na kujije ga kisasa lazima kwanza nyumbani/
ila chonde chonde usilivamie jiji kwa pupa/
mziki mnene mtaa wa kongo fally ipupa/
wapo ambao wamebobea kwa hongo na uwizi wa mawazo bado hautambuliki lupango/
suala la ufisadi ukosefu kiinua mgongo unafanya morali ya utendaji kazi kuwa so low/
how we gonna survive this conditions is low average foreigner investor or billions illuminat chances/
ndio maan nageuza visa kuwa maisha amka mtanzania ndio muda wa kufikiria sisha/
one the incredible
soga za mzawa
hoja za kugawa
wenye fedha wakihonga kwenda moja nao sawa/
uzawa wagonjwa bado tunaingoja dawa/
nikionja je hawa wagonjwa nitapona nao?
vipi litaota zao langu mlipa kodi/
niliyekualika kw_ngu pindi ulipopiga hodi/
ukajiita kiongozi k_mbe mwanasiasa mwana si hasa uananidanaganya na mimi sasa/
maisha bora ni uongozi wengi tunaigiza wanajiingiza mpaka viongozi wa makanisa/
kisa hawalipi kodi wala ushuru/
bila hodi wako huru/
zaidi ya bodi ya takukuru/
uhuru kwa wajanja kwenye nyanja zao/
walishajipanga bila mikwanja hujalamaba chao/
biashara za magendo malengo masihara/
sera zitajenga vipi juu ya matendo ya hasara?/ aaah
wapo ambao wamebobea kwa hongo na uwizi wa mawazo bado hautambuliki lupango/

stereo
yooh
siwezi kukataa kwenye sanaa tuko tofauti/
umefika wasaa mcee napaza sauti/
ifike mbali sio mbaya hata nikishautii/
umoja usionekane tuu ntapofikwa na mautii/
endesha motokaa mii na baiskeli/
simple tuu navaa life tight kwelii/
kisa huyu kanyimwa yule kapata ndio kinachosababisha yanajengwa matabaka kati ya wasanii kati ya jamii/
eti flani hawezi keti alipoketi madee/
mara moco haelewani na p mcee umoja ni nguvu so tushake na hii/
teach bila kisomo umoja ni dhahabu/
leo na preach bila kikomo kwa hoja za vitabu/
bila kiko na mkongoja wa mababu/
hizi busara kwao wale wanaongoja majawabu/
nikki mbishi
baba malcom
yeah
aah
fanya mke na wtoto wafurahii/
sio unamwaga mbegu kila chocho na popo wanakudai/
bia na kitimoto nyumbani ukoko na chai/
ukishakuwa mkubwa tambua kuwa utoto haufai/
kaya ikikosa lakaa mzazi hupaswi kujikosha/
kwa kuvaa moka kuficha uduni wa ulipotoka/
huvumi lakini umo na nguzo ya uchumi ni mbovu/
basi usiombe isuk_mwe na mchumi mwenye upofu/
ona nyota ya kijani fuata uzazi wa mpango/
umudu mavazi,malazi,makazi kodi ya pango/
bili za maji umeme wa luku toa michango/
mlo kamili watoto wasiishie kuonja finyango aah/
malezi bora mtoto asiwe chizi j_po maandiko yanasema usimnyime mtoto fimbo/
isiwe tija akikosa bakora utadhani mwizi ama mkora aliyetia fora kwenye uhalifu/
mfunze awe nadhifu ajichunge kitakatifu/
mke sio golikipa,mume sio atm machine/
yakikufika wee shika jembe ukalime/
aah baba malcolm baba familia/
kwenye platform nadhani kila baba ananisikia/

end

كلمات أغنية عشوائية

كلمات الأغاني الشهيرة

Loading...