kalimah.top
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

rostam (tz) - kaka tuchati كلمات الأغنية

Loading...

oooii naona mtandao unakatika
upo kimya sana mkato au kunde imevunjika
na mtanyooka roundi hii
na hivi huwezi bila mimi?
unajikuta jay z oya unarudi lini?
kaka huku wamefunga mipaka
ila tiketi nilikata nirudi kabla ya pasaka
rudi ugeuze kisu sio
mwana wa kulitafuta mwana wa kulipata
round hii sio nunio, daraja la mkapa
k_mekucha hivi saa ngapi huko nipe takwimu
nimeamka nishaweka bundle namngoja umi mwalimu
anapambana yule dada
tanga nimewavulia kofia wametoa sanitizer za iliki
yaani ukipaka unanukia
hehehe corona nishai yaani bongo kila mtu daktari
masai kachemsha majani ya mpapai kanywa na sukari
guza hadi maski wanafua sijui ni nani kawafundisha
huku kuna dada kajif_kiza mashetani kayapandisha
tueke siasa kando, unajua uchumi unashuka
sio bongo tu hadi ngambo watu wamefunga maduka
hapa nawaza pesa ya bango benki walokopa wanajuta
tukisema tukae ndani na hii njaa si ntakufa
hali inatisha na umasikini, tunaoumia ni sisi
yaani bora ufe kwa ukimwi angalau utaandika urithi
kwa iyo hamna bata, sio kidimbwi, sio tipsi
kaka madanga yamekata so hazitimbi hizo piece
(chorus)
bwana wa mabwana mungu wa miungu
alpha na omega nani kama wewe
bwana wa mabwana mungu wa miungu
alpha na omega nani kama wewe

hivi unakaa jimbo gani au marekani
unajikinga vipi maana vifo vingi hadi siamini (mmmh)
au umesharudi upo zako horohoro nini
we bwana hebu niache mi nimeze chloroquine
umenik_mbusha kweli chloroquine ni dawa?
bado inafanyiwa uchunguzi ila haijadhibitishwa
ingawa ukinywa haitohatarisha ndio maana bado wanaigawa
mi ninakunywa maana nilishika uso kabla ya kunawa
eti unaweza ukawa nayo na usionyeshe dalili?
ewaah! uko sahihi, na kingine kuhusu hili ni kwamba
mgonjwa wa corona unaweza usimtambue kwa macho
so mtu yeyote unayemuona mpe mita mbili toka kwako
na hiko kivansileka ndo kinini baba wawili?
ni ventilator, ni mashine ka mapafu ya nje ya mwili
mmmh sijaelewa hebu nieleweshe kuhusu hili
naskia vinauzwa ghali basi viwe vingi muhimbili
okay, kirusi cha corona kinashambulia mapafu
ndipo zinaanza homa, kifua alafu
unashindwa kupumua na mwili unahitaji tafu
ventilator huingiza hewa na kuitoa iliyo chafu
tuepuke mikusanyiko ikibidi tukae ndani
tumeambiwa tujif_kize hivi ni dawa unadhani?
ngoja kwanza, hivi fumigation (mmmmh mmh)
baba ile inaua mende tu (hahaha wacha utani)
(chorus)
bwana wa mabwana mungu wa miungu
alpha na omega nani kama wewe
bwana wa mabwana mungu wa miungu
alpha na omega nani kama wewe

maisha ya upweke yanasumbua ila siku zinapita
yule mkewe itunze pete
mtayamaliza na uhakika kaka
ila hatua dua haina haja ya kusikitika
ila navyokujua hujazini miezi sita?
kiukweli mi mwaminifu ingawa jogoo anawika
mama ivan mbabaifu haku_cheat una uhakika?
kuna mchezaji wa yanga namwona anapita pita
nitamkata kata mapanga yaani namuua na namzika
oyaah wape nyumbani basi pesa ya matumizi
kaka nitoe wapi na show hakuna siku hizi?
hali imekuwa ngumu hakuna pesa kila kona
kila mtu unayemdai naye anasingizia corona
mbona sasa wanafunga shule na vyuo alafu bar hawafungi
mzazi atamlindaja mtoto na akirudi yuko tungi?
polisi india wanapiga watu wakisongamana
wao barakoa hawana, jua defender wamebanana
sasa wanatukusanya kutuambia tusikusanyike
ila wauguzi wanajitoa sana, dah mungu awalipe
wapinzani mnatangaza vifo walopona hamwatangazi
ah_ah wanasema w_ngeweka takwimu za wazi ingekuwa kizazi
kwa hivyo lockdown hakuna alafu umeona text niliyotuma?
ipi kwenye group mbona inbox hakuna?
ah naskia (nini?) koyuzeka mbochi
maana uliko uliko usiongee sana inatosha
hadi papai lina corona dah (kaka tuchati)
mmmh ina mbuzi vipi? (eeh eh kaka tuchati)
mwili umekufa ngazi (kaka tuchati)
poa mwanangu tuendelee kujif_kiza

كلمات أغنية عشوائية

كلمات الأغاني الشهيرة

Loading...