prof. jay - zali la mentali كلمات الأغنية
naamka asubuhi nipo chwiri tena mapema
nautoa mkeka sakafuni kisha naukunja vyema
nawaza nitakula nini mentali kisha naguna
naanza kujikongoja kichwa chini mikono nyuma
naelekea kilingeni nilikopaki mkokoteni
nasaga na rumba kimshazali nyie acheni
nawapa, “hi” machizi wananipa, “peace” tunafurahi (aah, vipi mzee, poa bro)
tunapiga stori nyingi walahi bila maslahi
mara napata zali napeleka kago uswahili
wananipa buku mbili dangaa chee n_z_sunda chini
wakati natoka huku kijasho chembamba kikinitoka
nikaona toto ya nguvu nikajikuta nimeropoka
“dada habari samahani naomba niulize swali”
akajibu, “maskini koma tafadhali hii ngoma ya gari”
“ehee unajua dada?”, “we vipi hebu nipishe”
“dada mbona mkali”, “we kinyago kubali yaishe”
nikasema inshallah hiyo yote sababu f_kara
nisije nikakubaka nitupwe selo nikawe kafara
nikaachana nae sehemu za nyuma akizitingisha
nilikula kwa macho hadhi yangu haikuridhisha
nageuza mkokoteni nakuelekea maskani
nikawapa stori machizi wakanicheka ikawa utani
siku moja nililemaa maskani sikuwa na tenda
na nilikuwa nikitafakari ni vipi siku itakwenda
k_mbе kuna gari ilikuja na kupaki karibu yangu
sikuweza kuisikia labda sababu ya njaa yangu
nilishtushwa ghafla na mlio mkali wa honi
nilipatwa na mshtuko na hofu kubwa moyoni
kuangalia pembeni ilikuwa imеpaki toyota surf
kulikuwa na sura ngeni ya malaika akaomba tafu
nilisita kunyanyuka kwa sababu nilikuwa mchafu
na alitoa elfu k_mi na alikuwa akitaka dafu
nilipokea hela, alichotaka nilimletea
akakipokea, tabasamu zito akanitolea
nilimpa chenji
“oh no, keep change, una mawazo mengi itakufariji weekend”
alikunywa maji ya dafu alitupa na kunikonyeza
niliganda kama nyamafu nikahisi alinibeza
alinipa busu la huba shavuni akanichombeza
“i love you”, akawasha gari akateleza
zali la mentali
limetokea wakati mimi n’na njaa
nikapendwa na demu mkali
na kuwaacha watu wote wakinishangaa katika mitaa
zilipita siku mbili nikiwaza kilichotokea
nikawaza yule ni mtu au jini amenitokea
potelea mbali uchawi hauendi kwa mentali
narudi nanyonya napuliza mentali nakuwa shwari
nabeba rumbesa nakatiza samora avenue
mara kwa ghafla mbele yangu inapaki toyota mark ii
oh, napanda ghadhabu mara nyingi sipendi dharau
naifuata gari kuanza kupaka, mara nahema juu juu
ah, ni yule mrembo
“maskini pole sana mzigo mbona mzito kweli utafika nao salama”
natabasamu
“oh, nimeshazoea mama na namshukuru mwenyezi mungu kwani hii ni kama karama”
anakuwa mnyonge anakata kucha anan’tazama
anaanza kulia anatoa leso anainama
namwambia, “bibie ni mara ya pili tunaonana
na sidhani kama ni mbaya iwapo tukifahamiana”
“naitwa vickie nina miaka 22
ni mtoto wa kipekee kwenye familia ya kitajiri”
“oh, naitwa jay ukiniita f_kara haukosei
na naishi kwa nguvu za macho siku zenyewe hazisogei”
alishuka toka garini na kusema, “jay nakupenda”
akaruka kw_ngu mdomoni nakuanza kupata denda
nilich0m_ka kwake na kuanza kurudi nyuma
“tafadhali mpenzi jay jamani nionee huruma
acha kubeba mizigo panda ndani kwenye mchuna
twende mbezi beach kw_ngu upepo unapovuma”
“sikiliza vick napenda tuwe marafiki
lakini hadhi yako hutakiwi kuwa na mtu wa dhiki
hata wazazi wako naaamini hawataafiki
tajiri na tajiri maskini sithaminiki
tafuta kibopa mwenzio ili usishushe hadhi yako
mimi sistahili hata kuwa kijakazi wako”
“tafadhali jay usitamke maneno hayo
naomba unielewe haya machache niyasemayo
hadi huu wakati mimi nimekupenda kwa dhati
ukikubali niwe wako nitajiita mwenye bahati”
“nimeelewa vick naomba niwahishe mzigo
tajiri ni mkorofi anan’subiri migomigo
na kila nikichelewa mwenzako napata kipigo
nasaga na rumba jua na mvua kwa mpigo”
tuliongea mengi akanipa hela za matumizi
sikuwahi hata kuziona nilikuwa kama chizi
niliacha kubeba mizigo penzi letu likaota mizizi
watu wa uswahili wakasema natumia kizizi
zali la mentali
limetokea wakati mimi n’na njaa
nikapendwa na demu mkali
na kuwaacha watu wote wakinishangaa katika mitaa
baada ya miezi mitano vick alipata ujauzito
tulifurahi sana mambo yakawa mpwito_mpwito
swala la kwenda kwa wazazi wake halikuwa zito
walifurahi sana kuniona tukafanya tambiko
walisema jay maisha ya vick yapo chini yako
tumefurahi mmpendana k_mlea ni juk_mu lako
ilipangwa mikakati kabambe ya kufunga ndoa
watu hawakuamini kama mimi vickie nitamuoa
ilifika siku ya siku mentali jay ndani ya jumba
na vickie ndani ya shela hakuna uchawi wala ndumba
tulishikana mikono ni nderemo na vifijo (halele!)
tukafunga pingu za maisha kanisani bila ya fujo
furaha isiyo kifani lilifanyika bonge la party
watoto wa uswahili walibeba wali kwenye mashati (du)
zawadi zilizagaa zilikuwa nyingi tena kemukemu
baba mkwe alitupa benz, kiwanda, nyumba na bm
acha zawadi nyingi kutoka kila sehemu
nilik_mbuka nikacheka nilivyoteswa na wale mademu
mambo swadakta nipo na vickie ndio my wife
kidume nang’aa wanajigonga shenzi type (shenzi type)
nilipokuwa arosto mlinikwepa kama ukoma
mambo juu ya mstari kunisalimu mnaona noma
sasa hivi napeta nabadili gari full kipupwe
mlio nicheka wanataka ardhi ipasuke
naelekea kilingeni kuwapa dili machizi w_ngu
tena mara kwa mara siwezi kuwacha asili yangu
vickie ni jay, jay ni vickie mustarehe
kutoka ndani ya dhiki, sa’ kila siku sherehe (ah_ha!)
zali la mentali
limetokea wakati mimi n’na njaa
nikapendwa na demu mkali
na kuwaacha watu wote wakinishangaa katika mitaa
كلمات أغنية عشوائية
- xate كلمات الأغنية
- дай дарогу! (dai darogu!) - д.с.п.г. (d.s.p.g) كلمات الأغنية
- wolves at the gate - the cure (redux) كلمات الأغنية
- ona mafalda - desaparecer كلمات الأغنية
- domi wolf - miuc كلمات الأغنية
- james bks - no unga bunga كلمات الأغنية
- gerardo casiello - mon désir, mon amour كلمات الأغنية
- asthma - miejcie się كلمات الأغنية
- other night fears - no one laughs كلمات الأغنية
- kylie minogue - what do you know كلمات الأغنية