kalimah.top
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

novicbcvm - gospel rap كلمات الأغنية

Loading...

novic bcvm – gospel rap lyrics
artist: @novic bcvm
t-tle: gospel rap
album: gospel rap | mixtape album
genre: 255 christian rap
rating:
•••••••••••
[verse 1:novic bcvm]
nimezunguka zunguka sijaona kama wewe
uliyemweka chini mjusi na juu ukamweka mwewe
u mkuu mfalme, falme na hata falme
you’re the alfa & omega ufalme wako wa milele
ulitupenda kwanza mfalme hupendelei
huk-mdharau mnyonge ambaye wengi hawamtetei
mbingu hunyesha mvua kwao wema na wabaya
na umeliweka jua wenye akili kuona haya
baba baba natangaza sifa zako
ninaimba rap kufikisha ujumbe wako
uwafikie watu wako wasikie neno lako
watubu wanyenyekee chini ya mkono wako
umeagiza neno lako lihubiriwe nchini kote
watu wapate sikia iwe ni kwa njia yoyote
iwapayo amani na kuwafanya waokoke
wavikwe utu upya ule wa kale uondoke
baba bariki rap na tuiimbayo pia
ile yenye nidhamu roho pia na nia
waimbaji wenye wokovu na tunda la roho pia
yaani ni upendo kiasi na hivyo vilivyo bakia

[verse 2:novic bcvm]
kila siku inapokucha ni bora afadhali ya jana
shetani hutoa makucha yanayo rarua hasa vijana
nguo za uchi miili wazi mtaani kwa wasichana
wanaita pamba gucci milegezo isiyo na maana
sio kaka wala dada wamekosa mwelekeo
hawataki sikia ibada shetani wampa vyeo!
starehe anasa kama ada ni uasi mamboleo
ni mara k-mi ya sodoma kilivyo kizazi leo
mwana mwenye hekima humfurahisha huyo babaye
bali mwana mpumbavu huwa mzigo wa mamaye
mheshimu baba na mama siku zipate kuwa nyingi
usimdharau mtu yeyote akushaurie jambo la msingi
kupinga pinga habari za mungu wewe koma
neno lake lahubiriwa kote nchini corner to corner
vipofu hupewa kuona, viziwi sikia vema
walemavu kutembea sijui utaokoka lini bwana!
ni time yako bwana yesu k-mpokea
humo moyoni mwako k-mwacha yeye kuku -care
mawili macho yako yote juu k-mwelekea
akufanye chombo kipya sasa na kuendelea

[verse 3:novic bcvm]
eloi, eloi, lama sabakthani?
alinena hayo yesu alipowambwa msalabani
alilia kwa sauti kisha akakata roho
hakuhofu hiyo mauti hakuthubutu ooh no!
alin’lilia mimi nawe, tuwe huru tukombolewe
tupewe nuru tuangaziwe nguvu za giza zisiwe nawe
tendo hili la ajabu, lil’fanyika kwa sababu
kufungua kipya kitabu nakiheshimu kwa adabu
msamaha ule wa bure, daraja fika kule, itwa wateule kuingia mji ule
yanywa maji yale, imba nyimbo zile, k-msifu yeye yule jana, leo na milele
napopita hupitika c’se bwana amenishika
sigeuki tazama nyuma mbele yangu ni hakika
mungu wa uhakika ananijua mimi fika
before kwa mama yangu tumboni mi sijaumbika
kila sekunde inapopita, pumzi nnavyovuta
nywele inaponiota -jicho lake hunitafuta
kwa sauti yake anakwita usichelewe kuitika
malango kufunguka nazo baraka kufurika
unangoja nini wewe leo hii ni siku yako
neno gani uhubiriwe kubadili maisha yako
amen naomba liwe hilo ndilo jibu lako
na mungu w-ngu akusaidie katika wokovu wako. x 2
@novic bcvm

كلمات أغنية عشوائية

كلمات الأغاني الشهيرة

Loading...