kalimah.top
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

mpinboya - wanune كلمات أغنية

Loading...

mapenzi

ni neno lililo fupi, lenye kina cha urefu
siezi sema w_ngapi, mamia kwa maelfu
hakuna mtapi tapi, alo dumu maradufu
si kingine ni mapenzi, ni wengi yame waliza

maumivu ya mapenzi, ni zaidi ya msiba
waeza k_mwaga chozi, ukakaza kwa msiba
kitu ingine mapenzi, usiudharau mwiba
ni mapenzi si kingine, yatutoayo machozi

ning’ini ukajinyonga, ukaacha familia
na gari ikakugonga, kwa mapenzi kuwazia
ukaenda kwa waganga, penzi lipate tulia
si kingine bali penzi, ndilo latuangamiza

halijali uf_kara, wala alietajiri
mapenzi yana mkwara, nidhahiri sio siri
penzi huleta madhara, halichagui umri
ni mapenzi si kingine, yaletayo ubaguzi

waeza ishi mwenyewe, dunia kaona chungu
ukapatwa na kiwewe, ukapita na virungu
watu kawaona mwewe, ukamkufuru mungu
ni haya haya mapenzi, yanotutia uchizi
kashindwa kula kulala, ukawa kama kituko
lawama k_mpa swala, ukaonwa nizumbukuko
kila kitu una zila, hupo huku kule uko
ndivyo yalivyo mapenzi, yakubali matokeo

pеnzi lina vingi visa, furaha pia visasi
moyoni likitakasa, upatepi wasiwasi
usombe likatikisa, ndugu utabwia nyasi
ndivyo yalivyo mapenzi, kikubwa kujikubali

pеnzi pupa halitaki, ukajitia mjuzi
uje vaa penzi feki, ikawa kwako kitanzi
penzi tamu kama keki, zaidi ya maandazi
ni mapenzi haya haya, ukweli nimeeleza
mwamba lakabu
mpinboya sanii
mpin bo ya

jameni nadai mnisapoti si waona mistari ipo
@topfans

كلمات أغنية عشوائية

كلمات الأغنية الشائعة حالياً

Loading...