ghafla - nainuka tena كلمات الأغنية
chorus (shine nuny)
twende mbele turudi nyuma hata nikianguka tena
nafufua ndoto zangu nione kesho njema
nainua macho yangu nione mbingu vyema
natetea ndoto zangu nami niishi vyema
ona nainuka tena x2
natetea ndoto zangu nami niishi vyema
verse 1(ghafla)
nimetoka kwenye shimo nikiomba wasionijua wanivute
maana rafiki walikimbia wakijua lazima nife wakisubiria wanizike
unajua ni jinsi gani naishi nao?
nafurahi toka moyoni ninachopata nakula nao
jamaa
sikuweza simama haraka ila nilijiinua kwa sala
aina ya tunda la adam alinionyesha nikala
aliniponza tukaf_kuzwa eden kufika huku akaniacha
hii ni aina ya wanawake niliowapata
nitakula nao sahani moja
usijali itatutosha
nitaenda nao sambamba usidhani watatoka
ni nani kaua mbwa wa john wick
ni nani anaehamasisha kama mimi huku street
nimeitupa degree maana hata walimu hawakuniamini
sisambazi cv nilichukuliwa muhuni ofisini
nasimama na ninachoweza
ona nainuka tena
bila kioo najiona vyema
nabeba ndoto za moto n_z_changanya na upendo n_z_pooza kwa pesa
naamka toka ghetto na nguvu mpya tena
hii itahamisha milima isipofufua uzima
mapambano yanaеndelea ushindi kwetu lazima
ni salama ila inatisha
kila alama ya maisha tunaitazama kwa kina..ooh lord
chorus (shinе nuny)
nafufua ndoto zangu nione kesho njema..
ona nainuka tena x2
natetea ndoto zangu nione kesho njema
verse 2 (ghafla)
nainuka tena jembe jipya ardhi ile ile
mavuno ni kitu chetu majuto si mwana kwetu muda w_ngu acha nile
nina njaa nina kiu
sio ndoto za usiku sina njozi hazipo
siogopi tatizo
mara ngapi nimeruka miba wakanitegea misumari
mara ngapi nimeachwa njia panda nikaambiwa siwezi vuka mto nimetukana mamba
nilichukua tahadhari
ninachoogopa ni kuvunja daraja najua nitarudi baada ya safari
historia ya mama kwenye mashamba ya miraba
tulilia na baba kuhusu chai na ada
tuliumia kwa mitaa kwa utumiaji wa ngada
tulisoma kwa uchungu ila roho haikuwepo hapo
ila sababu nilitaka kuona tabasamu la mama,nilikazana
ila akili yangu ikiwa studio napush
tulijaza mistari katikati ya daftari mwalimu usiniulize tuliishia wapi
tuliamka shkamoo mama shkamoo baba na hamsini hamsini za kalmati
hivyo usiniulize nitakula wapi
tulivusha mchana tukisubiri mama arudi na zawadi
nilitamani kula jirani ila ndugu zangu watakula wapi
nitajisikiaje yaani
mimi nacheka wao w_n_lia njaa kali
hivyo nilirudi tukatazamana
huku meno yakiumana
sasa utaniambia nini kuhusu dhiki
utaniambia nini kuhusu mziki
utaniambia vipi niache mziki
hivi unajua nimekuwa vipi?
sina chochote cha kupoteza
jicho linatazama rizki na macho yanatazama fedha
nainuka tena na mitaa
bora mara nyingi ya unavyonijua
na watu w_ngu nawachukua
wala siogopi unavyonichukulia
wala siogopi ukinichukia
sina hofu hata safina iliacha watu
huu mchezo nao ni rafu ila nina uhakika nitatusua kama hujanijua
yeeah
chorus (shine nuny)
twende mbele turudi nyuma hata nikianguka tena
nafufua ndoto zangu nione kesho njema
nainua macho yangu nione mbingu vyema
natetea ndoto zangu nami niishi vyema
ona nainuka tena x2
natetea ndoto zangu nami niishi vyema
كلمات أغنية عشوائية
- hairspray - (you're) timeless to me كلمات الأغنية
- chrystian & ralf - de cara cheia كلمات الأغنية
- harpa cristã - sublime e grande amor كلمات الأغنية
- voz da verdade - momento de glória كلمات الأغنية
- tonico e tinoco - brasileiro كلمات الأغنية
- bee gees - love hurts كلمات الأغنية
- tonico e tinoco - dois corações كلمات الأغنية
- christina aguilera - i'm ok كلمات الأغنية
- carlos do carmo - cantiga de maio كلمات الأغنية
- tom zé - senhor cidadão كلمات الأغنية