fivara - taswira mpya كلمات الأغنية
[intro]
yeah
a piece of pie muzik
nahmsehhhh…
[verse 1]
heshima kwa viongozi waliotangulia, kazi kwa waliobakia
kuyaendeleza mema hiyo ndio kazi iliobakia
wananchi tunaamini nyie mnaona njia
mtufikishe nchi ya ahadi, hiyo tanzania
mliotuambia kwenye sera na kampeni
tunaombeni zisiwe sera tu, ebu fanyeni
rushwa, ufisadi ebu punguzeni
halafu viwanda na miradi ebu fufueni
matatizo ya wakulima na watoto na shuleni
kuhusu afya mfanye hima, suluhu tafuteni
ndio mnajitahidi kupunguza foleni
lakini vipi wamachinga, wasuk_ma mikokoteni?
mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni
sio mzawa hapati chake halafu anapata mgeni
kujivunia nchi yetu isibaki kuwa usemi
ila uzalendo uwe wimbo, kila mmoja awe na deni
[chorus]
ninayoiona ni taswira mpya
na kila nikilala naliona taifa jipya
ni kama tumеpata dira mpya
cha msingi tuwe imara kwenye maono kufika
ninayoiona ni taswira mpya
na kila nikilala naliona taifa jipya
ni kama tumеpata dira mpya
cha msingi tuwe imara kwenye maono kufika
[verse 2]
heshima kwa kiongozi alietangulia, kazi kwa aliofuatia
kuyaendeleza mema, hiyo kazi aliyokuachia
nchi nzima watu wote tunakuangalia
mwanamke wa kwanza kuandika historia
makubwa mengi toka kwako tunatarajia
tangu ule kiapo usukani ulipokamatia
tunaamini hata wapinzani watafurahia
utarudisha demokrasia na umoja pia
sio kuendekeza u_chama, kujenga uhasama
rudisha uhuru wa habari, tutakushukuru sana
hakikisha utawala umesimama
tujali kweli wanyonge, tunalala tumesimama
vipi mfumuko wa bei j_po uchumi wa kati?
tuonyeshe mwelekeo wa maendeleo tuwe safi
pia tunaomba utuongoze kwa haki
ili amani, tumaini tusiulize “viko wapi?”
[chorus}
ninayoiona ni taswira mpya
na kila nikilala naliona taifa jipya
ni kama tumepata dira mpya
cha msingi tuwe imara kwenye maono kufika
ninayoiona ni taswira mpya
na kila nikilala naliona taifa jipya
ni kama tumepata dira mpya
cha msingi tuwe imara kwenye maono kufika
[verse 3]
kila mmoja afanye wajibu wake
ni kama swali kila moja na jibu lake
kila nchi ina mbichi na mbivu zake
hivyo struggle hazifanani, kila moja mbinu yake
nikiangalia yetu na miundo mbinu yake
naiona mbali tukijali umuhimu wake
vipaumbele tuwape watu wake
misemo tuache, mtaji wa maskini nguvu zake
elimu, sayansi vyema kuzingatia
tukiweka nia lazima tutaiona njia
mshikamano haijalishi dini au chama
tusiwafuate wamagharibi wanasubiri tukipigana
tuhakikishe tunasimama tunajitegemea
tuweke kando uhasama taifa kuendelea
na heshima kwa viongozi waliotokea
tubebe mazuri tuache maovu walipokosea
كلمات أغنية عشوائية
- screams in silence - watch me bleed (it's what you like to see) كلمات الأغنية
- exodus1900 - tundra:techno_biome.mp3 كلمات الأغنية
- +junk!e - bread 2 كلمات الأغنية
- themarsshow44 - the sun كلمات الأغنية
- farzad farzin - man be jahanam كلمات الأغنية
- coucou chloe - ice castles كلمات الأغنية
- roberto velázquez martínez - aquí كلمات الأغنية
- bethany music - when we praise (live from new orleans) كلمات الأغنية
- greenbeard - battleweed كلمات الأغنية
- sinn - rage كلمات الأغنية