kalimah.top
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

fid q - kemosabe كلمات الأغنية

Loading...

niliamini mapene hayatoshi..na niki-hustle siyakosi/
sababu.. sipo kwenye loss na life simple huwa hai-cost/
kwahivyo nikaenda dar na treni… of thoughts../
sikwenda kuzubaa au kushangaa nikusaka chapaa boss/
sikutaka kuivaa mikosi..nilitaka kuivaa mikoti/
sikuwa na p-ssport..p-ssword.. pin..lakini ni crack codes/
walionisapoti wote siwaoni kwa line/
wakini-approach ili nifungue pochi ya noti tu-shine..hatuko fine/
je mimi ni kaka mubaya…? kaka aso haya../
kaka..? huniitaga nakaaya/
mama c huniita brother bila shaka.. mozaya/
niko sick & tired of being sick & tired/
na huu ni mwaka wa ndui/ sitaki upele urudi tena.. mnachotaka sikijui/
nashukuru hamtopata mbawa ikiwa mtaupata huo uchui/
mnautaka uadui? mnayempaka ni mtata.. makaka hamkui?
mmeendekeza hila.. legeza hasira za harakati/
mie nita-ball…. hata kwa mpira wa makaratasi/
unaweza ukahisi mie napita tu.. kwakusahau mie nina-hustle/
nimezaliwa afrika.. ugumu wa maisha umenifunza ku-struggle/
ukiwa idle.. unamu-attract shaytwan (shetani)/
kichwani nina msahafu na bible.. life ni zaidi ya ku-have fun/
kwani.. kila kicheche anajiona ni mzima/
na njia pekee ya kuepuka ngoma ni kugoma kupima/
ikiwa maujuzi haya hayakugusi.. itanilazimu nikuelewe/
sometimes hata kamusi.. huimiss tafsiri yenyewe/
nalindwa na dua za mama.. tangu baba simjui/
namfanya adui mwenye njama aache drama na akue/
ili ajijue kabla hajakwama huko mrama asitue/
ajikwamue kwenye lawama.. yenye maana yamchukue/
kisha anaiombee mimi ili nifaidike kwa hizi mbio/
siamini kwenye umasikini hivyo sihofii mafanikio/
ndiyo.. mie ni leo kwahiyo sifikirii kushindwa/
zingatia kauli hiyo hausikii inaashiria ubingwa?/
mie ni mbishi.. muulize nikki – hatopinga/
na hata kama ningekua mbuzi ningelala chaka la simba..

كلمات أغنية عشوائية

كلمات الأغاني الشهيرة

Loading...