dizasta vina - the verteller (official album intro) lyrics
inafaa kunena
inafaa kunena labda ni muhimu sijui
labda kusimulia si karama kama wanavyosema
ikiwa msimuliaji huingia hatarini
labda kweli baraka ni laana njema
wasikilizaji nasikia wana ndoto na wenyewe
si uongo
hadithi nzuri ndo’ kilele kwa wasikilizaji
ila ndoto ya msimuliaji
ndoto ya msimuliaji ni kulindwa milele
kwanini azibwe mdomo wakati ubongo unapiga kelele?
si lazima msimuliaji apazwe la hasha!
atandikiwe majani au aandikwe kama mwanasiasa
lakini lengo lake awe huru msimuliaji atambe
alindwe ili waovu waonyeswe, mashujaa watangazwe
ona kuna wasimuliaji hukwepa pande tupu
yani baada ya mitaji husimulia upande wa wenye nguvu
wapo wabinafsi wanaotangaza jinsi asili ilivyowahusudu
husimulia walivyoshinda vita wakigombea asali na wadudu
swali ni je? , nani atasimulia hadithi ya wadudu?
nani atasimulia kua si mara zote mchukua asali alimsulubu mdudu?
nani atasimulia hadithi ya shetani, baada ya kusikia upande wa mungu?
baada ya kusikia upande wa mungu
waungwana k_mbukeni ya muhimu na ziada
k_mbukeni ya uchumi jamii na siasa
lindeni ghala la chakula na maji
lakini msisahau k_mlinda msimuliaji, ni afya
j_po kuwa msimuliaji si alama ya taifa
lakini fikiria mtu ambaye yupo tayari kulipa gharama ya maisha
msimuliaji hukuk_mbusha ulipotoka ujuе unapoenda
na hiyo ndio faida
labda uk_mbuke ya mdimu na majoka
au simulizi za mizimu ya mloka
au tarihi ambazo ni historia za kuziheshimu
maana asiyеijua historia, huweza kurudia makosa
msimuliaji hachagui upande maana hapendi kupotoka
hafungamani na misalaba au alama za mwezi na nyota
alama za wasimuliaji walioidongosha kheri
waliookota sifa wakati wakiidondosha kweli
wakati wakiidondosha kweli
enyi wa khaki kijani na manjano
mmeona nyekundu ile pale?
haijaja pale leo ipo tangu kale
msiruhusu iwaguse
si kwakua hamna hadhi
la hasha
ila ile rangi anaifahamu msimuliaji
ile rangi ni damu iliyomtoka au k_mrukia
na mchanganyiko wa pande zote za dunia
anaijua leo, aliijua jana
hajaisoma au kuisikia
aliipata wakati akitafuta vya kusimulia
na ni hivi anavyotaka kukusimulia leo
nyakati za katikati kwenye eneo la ukanda wa kidachi
zilizaliwa lugha tatu, lugha ghafi
na kati yao ilikuwepo lugha iliyoitwa lugha ya watu
kwenye ukanda huu msimuliaji hakuitwa narrator au story teller kwa kiingereza
hakuitwa erzahler j_po kuwa ukanda huu ulikuwa karibu sana na ujerumani
hakuitwa rawi kwakua huu ukanda haukuwa wa kiarabu
msimuliaji aliitwa the verteller
kama christopher hitchens
ama professor laurence krauss
ama shaaban robert
ama francis scott key fitzgerald
ama chimamanda ngozi
ama fred saganda
ama alice walker
ama octavia burtler
ama lufufu mkandala
ama rainfred masako
dizasta vina, mabibi na mabwana
ni the verteller
كلمات أغنية عشوائية
- 2pac - unreleased songs [discography list] lyrics
- 24kgoldn - city of angels (nitro remix) lyrics
- hjemfart - vær du mig nær lyrics
- frayer flexking - rakety jak pizza lyrics
- stefano rosso - ragazza sola lyrics
- j coyn drive - brb (scene) lyrics
- lil dusty g - 666 lyrics
- motherfolk - somewhere in the middle lyrics
- davy's grey - road to your mind lyrics
- awkward marina - lazy ass bitch lyrics