dizasta vina - a father figure (official album intro) كلمات الأغنية
natazamwa kama mgongo
wa kuegewa kama chombo
nikitegemewa na watoto
lakini kwa ndani mi’ ni mtoto pia
mtoto wa katikati
njiapanda kati ya
ukweli na uongo
ukubwa na udogo ama
upofu na uchongo
ama pumbazo na mwongozo
katikati ya uhalisia
na mategemeo
karibu na jitihada
mbali na egemeo
sina hesabu ya mafanikio
kila kitu ni juk_mu na uwepo w_ngu
ndio huk_mu yangu ya leo
sina cha thamani nilichorithi
ila nilichonacho ni k_mbuk_mbu ya simulizi
na picha nilizokuwa nazo
nilizopewa na wavuja jasho
wasakatonge wa mwanzo kwahiyo
nigawie masikio yako
macho yalinipa tishio lenye manufaa kw_ngu
maana nilishuhudia kufanikiwa na
kushindwa kwa mashujaa w_ngu
lakini shuhuda zilinifunza
zilinifunza kuhusu mashujaa
wa karibu na mbali
wenye nasibu za ghali
au watabibu wa kuponya hali
na nguvu ya kuf_kuza shali
za wadhalimu na waharibifu
wenye visu vikali
mashujaa walisisimua sana
lakini wapo kadhaa waliokufa
na hawakuacha alama
nilifunzwa kuhusu hawa
hawa mashujaa walipanda maua
wakilea vyema yakachipua
na wengine usingizi ulipowachukua
wadudu wala mizizi wakaf_kua
machache yaliyofanikiwa kukua
ndege waliyachukua
na mengine hayakuwa mahala pema
kwahiyo yalichomwa na jua na kuungua
oooh hujui walimwengu walisema nini
kuhusu hawa shujaa w_ngu walioshindwa
walisema kaharibuu
kwakuwa shujaa kwa walimwengu
ni yule anayeweza wakati akifanya
lakini sio anayeshindwa wakati akijaribu
kwa walimwеngu shujaa
ni yule mwenye nguvu
asiyеtoa chozi wakati wa uchungu
asiyekosa au anayeonekana mtukufu
kwa walimwengu ushujaa ni
kuweza na sio kuthubutu
kwahiyo wakati sherehe za mashujaa
wao zikipikwa kuchochea
hadithi za mashujaa w_ngu
zilizikwa na kupotea
kwakuwa mashujaa w_ngu
hawakuvaa suti zenye nakshi na kuita
hawakuwa na viatu vya kung’ara hivyo
hawakupendeza kwenye jarida
ni kama walipima ushupavu wa mashujaa
kwa kuangalia afya za maua
bila kujua afya za maua sio ubora
wa anayeyajua pekee
lakini kuna jua na mvua na ni
ubashiri wa kujua lini vinakuja
uhakika ni kesho, kesho yenye giza
na hakuna anayeitambua
shujaa w_ngu alileta mlo mmoja
kuhakikisha siku haipiti, na aliweka
tofali moja wakati wa kujenga msingi
alif_gia barabara alipambana na
uraibu kama kamali, ulevi na madawa
ila hadithi yake haikuvutia gazeti
sio sawa
ni vile nimeanza kuwa kama shujaa
w_ngu nimegundua kuwa sijamaliza kujua
ni kama nimeanza kulea wakati sik_maliza kukua
natamani kuwa shujaa mzuri
lakini nipo hapa kujifunza
na pa kuanzia sipajui
sipajui maana maelekezo ni mengi saa hii
mara jikaze wewe, baba halii
mara utapoteza nafasi, watu hawatanii
mara kwanini usifanye kama nanihii
ona watoto wake wamenanihii
bahari ya elimu ni pana kuushinda upeo
kulia matarajio, kushoto mategemeo
bado najifunza sipo mbali
ila sijui lini nitakuwa tayari
inaniwia kuweka kipimo
cha kujua kipimo kiundani
kupima usahihi wa wito
ninaposema hadharani
unawaandaaje watoto kwenda mitaani
kwa sababu kuliko kuwa mkata maua vitani
ni bora kuwa mwanajeshi kwenye bustani
nini maana ya kuwa baba
ikiwa bado najifunza
kutosherehekewa nikishinda
ila kusakamwa nikianguka
hata nikipendwa au nikichukiwa
ni sawa ila si vyema nikapuuzwa
labda ninachelewa ila ni vyema
nimejua kuwa baba hazaliwi
anaundwa
كلمات أغنية عشوائية
- ex libris - dawn of sugars كلمات الأغنية
- waylon payne - what a high horse كلمات الأغنية
- tragic hero - by your side كلمات الأغنية
- katastrophical - air monarchs كلمات الأغنية
- nasty c - palm trees كلمات الأغنية
- optimistic - optim كلمات الأغنية
- zebo - kinder bueno كلمات الأغنية
- khazala - tagda hoja jatta كلمات الأغنية
- mary chapin carpenter - old d-35 كلمات الأغنية
- jotta a - o teu chamar كلمات الأغنية